Monday, April 23, 2012

Jitu zima laishi kama mtoto

Mwanaume mmoja (Jitu zima) nchini Marekani mwenye umri wa miaka 31, amekuwa akiishi kama mtoto mchanga kwa muda wa miaka 18 iliyopita huku akivaa nepi, kunyonya vidole na kucheza michezo yote ya watoto wa miaka miwili.Pamoja na kutimiza miaka 31, Stanley Thornton huku akiwa na umbile kubwa na uzito wa kilo 133 na urefu wa mita 1.67 bado anaendelea kuigiza maisha ya kitoto ambayo anayafurahia.
Akiongea na gazeti moja la nchini kwao, Stanley alisema kuwa anafurahia sana maisha hayo na haoni sababu ya kuwa mwanaume mkubwa kutokana na umri wake.


Stanley analishwa kama mtoto mchanga ambapo amekuwa akiwaajiri wanawake mbalimbali kumhudumia kama mama yake, wakimlisha chakula kwa kijiko, kumuimbia na kumfanyia kila anachostahili mtoto kufanyiwa.
Cha kushangaza Stanley ana fedha za kuwaajili akina mama, anazozipata kutoka serikalini ambako ana shughuli maalumu ambayo haikutajwa. Hivi karibuni Stanley alijitangaza katika televisheni kuwa anatafuta mama atakayekaa naye muda wote.

No comments:

Post a Comment