Monday, April 23, 2012

PAMOJA NA TETESI ZINAZOENDELEA SAJUKI BADO MZIMA INGAWA HALI YAKE YA KIAFYA SIO NZURI

UKWELI ni kwamba, staa mkubwa wa filamu za Kibongo, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ anaumwa,
Hali ya Sajuki imeendelea kuwa mbaya akidhoofu mwili siku hadi siku kutokana na kusumbuliwa na tatizo la uvimbe tumboni kwa muda mrefu sasa.

Aprili 15, mwaka huu Sajuki na mkewe Wastara Juma walifanya sherehe ya 40 ya kumtoa mtoto wao, Farheen ambayo ilihudhuriwa na waandishi wetu waliomshuhudia msanii huyo akiwa amedhoofu sana.
Pichani juu: Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’  (mwenye miwani) akiwa katika sherehe ya 40 ya kumtoa mtoto wao, Farheen iliyofanyika Aprili 15, mwaka huu.

Kwa mujibu wa mkewe Wastara, Sajuki alipokwenda katika Hospitali ya Apollo nchini India hivi karibuni alipewa dawa za kutumia kwa muda ambapo mwezi ujao (Mei) alitakiwa kurejea tena nchini humo kwa ajili ya matibabu zaidi.

No comments:

Post a Comment