Sunday, April 29, 2012

Pamoja na Kuugua Sajuki aendelea kupiga mzigo

Licha ya kwamba afya ya msanii wa filamu za Kibongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ bado hairidhishi kutokana na maradhi yanayomsumbua, juzikati staa huyo na mkewe Wastara Juma walinaswa ‘lokesheni’ wakiendelea kurekodi filamu yao.

 

Sajuki amekiri kuwa afya yake bado siyo nzuri lakini ameona badala ya kukaa ndani ni vyema akajishughulisha ili kukabiliana na ugumu wa maisha.
“Bado hali yangu si nzuri lakini kama mtu unaumwa na huna kitu kingine cha kukusaidia katika maisha lazima uwajibike, naumwa lakini siwezi kukaa nyumbani kwa sababu kila dakika moja ya maisha yangu inahitaji fedha,” alisema Sajuki.
 

Naye Wastara alisema kuwa, afya ya mumewe bado hairidhishi ndiyo maana wameamua kuingia mzigoni ili kuhakikisha wanapata fedha kwa ajili ya matibabu.
 “Kama unavyomuona mume wangu, kimsingi anaumwa na zinahitaji fedha kwa ajili ya matibabu yake na kujikimu pia, ndiyo maana unatuona tumeamua kuendelea na shughuli zetu za kisanii kwani bila kufanya hivi tutakwama katika mambo mengi.
 
“Hata hivyo, bado tunahitaji msaada ili tuweze kufanikisha matibabu ya Sajuki ambaye tunatarajia kumpeleka India haraka iwezekanavyo,” alisema Wastara.

No comments:

Post a Comment