KAMATI ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imependekeza wabunge
watungiwe kanuni zinazohusu maadili ya wanasiasa hao ambazo zinaweka
viwango kwa mienendo ya wabunge pale watakapokuwa wakitekeleza majukumu
yao ya kibunge wawapo nje na katika eneo la Bunge.
Kamati hiyo inaeleza kuwa kwa sasa maadili ya wabunge ambayo
yanasimamiwa kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, ambayo
kwa madhumuni ya usimamizi bora wa maadili ya wabunge, sheria hiyo
haikidhi haja ikiachiwa itumike peke yake.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hassan Ngwilizi, kwenye taarifa hiyo
anaeleza kuwa uzoefu unaonesha kuwa baadhi ya mabunge katika Jumuiya ya
Madola tayari wana kanuni za maadili na mwenendo wa wabunge ambazo
utafiti unaonesha kuwa kwa kiasi fulani kuwepo kwa kanuni hizo
kunaongeza imani ya wananchi kwa mabunge yao.
Malengo mengine ni kuwafanya wabunge kuonesha viwango vya juu vya
maadili katika kutekeleza majukumu ya umma hususani wanapokuwa
wakiisimamia Serikali.
No comments:
Post a Comment