Friday, April 27, 2012

Furaha yamtoa Tundu Lissu MachoziWakili wa waleta maombi ya wana CCM, Godfrey Wasonga, akitafakari kwa hisia kali muda mfupi kabla ya kesi ya kupinga matokeo yaliyompa Ubunge Tundu Lissu, hayajatangazwa leo Mahakamani. (Picha zote na Nathaniel Limu)Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki CHADEMA,Tundu Lissu, akilia kwa furaha muda mfupi baada ya Mahakama Kuu, kutupilia mbali maombi yaliyotolewa na Shaban Selema na Pascal Halu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupinga watokeo yaliyompa ushindi wa Ubunge, Mbunge huyo. Mbunge wa viti maalum Kataru, mkoani Manyara, Rose Kamili (anayeangaalia kamera), akilia kwa furaha pamoja na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu, muda mfupi baada ya Mahakama Kuu, kutupilia mbali pingamizi la kupinga matokeo yaliyompa ushindi wa Ubunge, Tundu Lisu,  leo mkoani humo


Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu, akifutwa machozi na mke wake, wakati wakitoka nje ya Mahakama Kuu, baada ya Mahakama hiyo, kutangaza kuwa ushindi wake huo ni halali.


Baadhi wa watu waliohudhuria kusikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Tundu Lisu kuwa Mbunge, wakifurahia ushindi huo, muda mfupi baada ya maamuzi hayo kutolewa.
.

No comments:

Post a Comment