Monday, April 23, 2012

Zitto aomba Bunge la dharura kumjadili Pinda

Leo wakati Zitto anawasilisha hoja yake ya kutaka kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu pamoja na kuiwasilisha misingi ya maombi yake ametumia kanuni ya 27(4) ambayo inataka kuitishwa kwa Bunge la dharura na mwenye mamlaka hiyo ni Spika wa Bunge .

Kanuni hiyo inasema kama ifuatavyo; "Endapo manufaa ya Taifa yatahitaji kuwa Bunge lisikutane tarehe ile iliyowekwa kwa Mkutano utakaofuata,bali likutane tarehe ya mbele zaidi au ya nyuma zaidi,basi Spika anaweza ,baada ya kushauriana na Kamati ya Uongozi ,kuliita Bunge likutane tarehe hiyo ya mbele au nyuma zaidi"

Kifungu hicho kimetumiwa na hivyo kwa kuwa Waziri Mkuu katangaza Bunge kukutana tarehe 12/06/2012 basi kuna uwezekano mkubwa likakutana mapema zaidi ili kujadili hoja hiyo.

Msingi mwingine wa hilo ni kutokana na ukweli kuwa kitendo cha waziri mkuu kuendelea kuwa ofisini huku akijua kuwa bunge linaweza kumjadili wakati wowote kinamfanya akose ujasiri wa kufanya maamuzi ama kuweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na hivyo kudidimiza uchumi wa taifa , au hata kufanya maamuzi akijua kuwa wakati wowote anaweza kuondolewa.

naomba kuwasilisha.

No comments:

Post a Comment