Monday, April 23, 2012

FATAKI AFUMANIWA AKIW ANA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI

Alikuwa na gari ya serikali

WAKATI serikali na taasisi mbalimbali zikihamasisha kuwalinda wanafunzi kutoka kwenye mikono ya wanaume wanaofanya mapenzi na wanafanzi, ‘mafataki’, Mustafa Kachenga (39), mkazi wa Kiluvya, jijini Dar es Salaam amenaswa gesti (jina tunalo) akiwa na mwanafunzi wa kidato cha pili.

NI ASUBUHI SIKU YA KAZI
Tukio hilo la aibu ambalo lilishuhudiwa na baadhi ya majirani, lilijiri saa tano asubuhi ya Aprili 16, 2012 ndani ya gesti hiyo maarufu iliyopo Manzese, jijini Dar es Salaam.
Habari zinasema, Kachenga ni dereva wa kigogo mmoja Wizara ya Ujenzi na kwamba, siku ya tukio alimpeleka bosi wake huyo kwenye semina na kumwacha kwa maelekezo ya kumrejea jioni.

POLISI, MAPAPARAZI WAINGIA KAZINI
Mara baada ya kupata taarifa hizo, timu yetu ya mapaparazi ilifunga safari mpaka Kituo cha Polisi Urafiki, Ubungo na kutoa taarifa ambapo askari watatu wasiokuwa na sare walitolewa kwa ajili ya msafara wa kwenda kumnasa fataki huyo.
Kwa kutumia msaada mkubwa wa chombo hicho cha dola, uongozi wa gesti hiyo ulipewa taarifa, chumba namba tano kikagongwa na kufunguliwa na mwanaume huyo aliyejitupia taulo kama yuko kwake Kiluvya ambapo aliwekwa chini ya ulinzi.
Mwanafunzi huyo anayesoma Sekondari ya Kiluvya, alikutwa akiwa mtupu juu ya kitanda, alishtuka kwa ugeni wa ghafla na kuanguka sakafuni akijifanya amepoteza fahamu ingawa haikuwa kweli.

ETI MWANAUME AJITETEA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwanaume huyo aliyekuwa na gari la serikali namba STK alipobanwa kuhusu uwepo wake na mwanafunzi ndani ya gesti hiyo alisema amekuwa akimsaidia kumsomesha hivyo na yeye huwa ‘anasaidiwa mambo f’lani’.
Hata hivyo, jamaa huyo akaapa kuwa hatarudia tena baada ya kuligundua kosa huku, kama kawaida ya binadamu, akimlaumu shetani kuwa ndiye aliyemdanganya.

DENTI KILIO MUDA WOTE
Wakati mpenzi wake huyo akitaitiwa na maswali ya awali, mwanafunzi huyo mwenye miaka 16 alikuwa akichuruzika machozi muda wote.

SAFARI YA KITUONI
Maafande shupavu waliwatwaa wawili hao ndani ya usafiri wao sanjari na mapaparazi wetu mpaka Kituo cha Polisi cha Magomeni ambako walitoa maelezo na baadaye kuswekwa mahabusu kwa kila mmoja na jinsi yake.

No comments:

Post a Comment