Monday, April 23, 2012

KESI YA LULU YATAJWA KWA MARA YA PILI LEO MAHAKAMA YA KISUTU


 
 Mshatkiwa Elizabeth Michael |(17), ' Lulu'  akielekea kupanda ngazi na kupandishwa Kizimbani Kesi hiyo  ilikuja kwa ajili ya kutajwa  Upelelezi haujakamilika hiyo ni kwa mujibu wa Wakili wa Serikali Elizabeth Kaganda alisema mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Rita Tarimo  hivyo kesi hiyo  itatajwa tena Mei 7 mwaka huu. Mtuhumiwa amerudishwa rumande.
 
 
 
Akisindikizwa .


 Mshtakiwa akipanda ngazi kuelekea Kizimbani ambalo kesi yake ilitajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam huku akiwa katika ulinzi kutoka kwa askari  Magereza.
 
 

Tofauti na ilivyokuwa  alivyo pandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza 'Lulu' leo alikuwa katika ulizni wa hali ya juu huku askari magereza wakiwa wamevalia mikanda  yenye mabomu ya machozi ikiwa ni katika kukabilia na rapsha ya aina yeyote ambayo ingeweza kutokea .
 
Kitu kingine ni kwamba msanii huyo alifika akiwa amevalia gauni refu na mtandio wake mwekundu walitu walijaa lakini siyo kwa wingi ambao wengi walitarajia kutokana na umaarufu alio nao Lulu hata kabla ya kufikwa na tuhuma  hizo za kesi ya mauaji ya aliyekuwa Msanii nyota wa Filamu nchini Steven Charles Kanumba.

No comments:

Post a Comment