KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), imeibua tuhuma za ufisadi wa Sh2.7 bilioni katika mradi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa Gongo la Mboto, Dares Salaam uliopaswa kufanywa na Kampuni ya East Africa Meat (EAMC).Mradi huo ulipaswa kutekelezwa kati ya mwaka 2005/06 kwa ushirikiano wa jiji na Manispaa tatu za Dar es Salaam. Akizungumza Dar es Salaam jana kwenye kikao kati ya kamati yake na watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mwenyekiti wa LAAC, Augustine Mrema alisema kampuni hiyo ya Malaysia ndiyo iliyoshinda zabuni ya ujenzi wa machinjio hayo. Mrema alisema katika mradi huo, Halmashauri ya Jiji iliingia mkataba wa kughushi na EAMC, huku wakiwashawishi watendaji kushiriki kwenye ujenzi wa machinjio hayo yanayodaiwa kuwa ya kisasa. Alisema kutokana na hali hiyo Halmashauri ya Kinondoni ilitoa Sh229milioni wakati ya Ilala ilitoa Sh364miloni, Temeke ilitoa Sh224milioni huku jiji likitoa Sh1.2bilioni. |
Thursday, March 29, 2012
Wabunge waibua ufisadi wa mabilioni D’Salaam
Shahidi akiri sheria ya uchaguzi ilikiukwa
SHAHIDI wa tano upande wa utetezi katika kesi ya uchaguzi mkuu wa ubunge
katika Jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam, Protas Tarimo amekiri
kuwa sheria ya uchaguzi ilikiukwa.
Wednesday, March 28, 2012
MATOKEO YA UCHAGUZI WILAYA YA BABATI YATENGULIWA RASMI NA TFF
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UCHAGUZI
WA VIONGOZI WA CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU WILAYA YA BABATI
TAREHE 27/03/2012
1. Kamati ya Uchaguzi ya TFF katika kikao chake
kilichofanyika tarehe 25 Machi 2012 ilijadili mkanganyiko na mgogoro
uliopo wilayani Babati kuhusu uchaguzi wa viongozi wa chama cha mpira wa
Miguu Wilaya ya Babati (BDFA).
Tuesday, March 27, 2012
Mkurugenzi Tanesco asikitishwa uamuzi wa POAC
MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), William Mhando, amesema ingawa suala la kupatiwa umeme lipo kwenye stahili za mkataba wake, hawezi kubishana na uamuzi wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) wa kuondoa jenereta nyumbani kwake.
Akizungumza kufuatia agizo la POAC kuondoa jenereta hiyo nyumbani kwake jana, ili aonje uchungu wa kukatika kwa umeme, Mhando alisema alishtushwa na hatua hiyo kwa sababu ni suala la mkataba, lakini hawezi kubishana na kamati.
“Mkataba ninao jana (juzi) nilishtuka kuhusu agizo hilo kwa sababu niliajiriwa na bodi na mwenyekiti wangu alikuwapo tutakaa tuangalie, lakini siwezi kupingana na maagizo ya kamati,” alisema Mhando.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa wa Bodi ya Tanesco, Jenerali mstaafu Robert Mboma, alisema watatii agizo la POAC la kuondoa jenereta la dharura lililopo nyumbani kwa mkurugenzi huyo.
Hesabu Mambo ya Ndani zawachefua wabunge
KAMATI ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC), haikuridhishwa na hesabu za
Wizara ya Mambo ya Ndani baada ya kubaini kuwapo upungufu uliosababisha
kupata hati yenye mashaka kipindi cha miaka mitatu mfululizo.
Waziri amkana Mkapa Arumeru
-Asema hakuna tatizo la Ardhi
-Waraka kumpinga Sioi wasambazwa
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodlucky Ole Medeye amewatetea walowezi wanaomiliki maeneo makubwa ya ardhi katika Jimbo la Arumeru Mashariki kwamba wanamiliki mashamba hayo kwa mujibu wa sheria.
-Waraka kumpinga Sioi wasambazwa
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodlucky Ole Medeye amewatetea walowezi wanaomiliki maeneo makubwa ya ardhi katika Jimbo la Arumeru Mashariki kwamba wanamiliki mashamba hayo kwa mujibu wa sheria.
Polisi akana Mahanga kukamatwa na masanduku ya kura
ALIYEKUWA Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Buguruni, Mark Njela (37)
ameieleza Mahakama kuwa hakupokea taarifa za aliyekuwa Mgombea wa Ubunge
katika Jimbo la Segerea kupitia CCM, Dk Milton Mahanga kukamatwa na
masanduku ya kura.
CCM, Chadema washutumiana Arumeru
SIKU chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa ubunge Arumeru
Mashariki, vyama vyenye ushindani mkali katika uchaguzi huo, CCM na
Chadema, vimeanza kutupiana maneno.
Polisi akutwa na bangi disko
SIKU chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kuagiza maaskari wanaokiuka
maadili ya Jeshi la Polisi na kulipaka matope kuchukuliwa hatua ikiwamo
kufukuzwa kazi, polisi mkoani Kilimanjaro amekamatwa akidaiwa kufanya
vurugu disko huku akiwa na misokoto minne ya bangi.
Wachungaji waonya viongozi serikalini
-Wasema hawana hofu ya Mungu, wakerwa na malumbano
VIONGOZI serikalini wameshauriwa kuacha kupoteza muda mwingi katika malumbano wakati Watanzania wakizidi kukabiliwa na hali ngumu ya maisha licha ya Taifa kuwa na rasilimali nyingi.
VIONGOZI serikalini wameshauriwa kuacha kupoteza muda mwingi katika malumbano wakati Watanzania wakizidi kukabiliwa na hali ngumu ya maisha licha ya Taifa kuwa na rasilimali nyingi.
CCM waisihi NEC iwalinde Arumeru
-Wadai vyama pinzani vimeanza mchezo mchafu
-Mbowe amvaa RC, adai CCM inakaribia kufa
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuwachukulia hatua za kisheria wanachama na viongozi wa vyama pinzani kwa madai ya kumdhalilisha mgombea anaewakilisha chama hicho katika uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki, mkoani Arusha, Bw. Sioi Sumari.
-Mbowe amvaa RC, adai CCM inakaribia kufa
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuwachukulia hatua za kisheria wanachama na viongozi wa vyama pinzani kwa madai ya kumdhalilisha mgombea anaewakilisha chama hicho katika uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki, mkoani Arusha, Bw. Sioi Sumari.
Mashahidi kesi ya Tundu Lissu watoweka
Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge wa jimbo la
Singida Mashariki, iliyofunguliwa katika Mahakama Kuu, jana iliingia
kasoro baada ya upande wa walalamikaji kukosa mashahidi.
Kesi ya Kibanda, Makunga yapigwa kalenda
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communication
Ltd, Theophil Makunga, jana alipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka
ya kuchapisha makala ya uchochezi yanayomkabili pia Mhariri Mtendaji wa
Gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda, na mwandishi wa makala hiyo,
Samson Mwigamba.
Mbowe: Kesheni kulinda kura
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Freeman Mbowe, ametangaza kuwa Aprili mosi ni siku ya mkesha wa kulinda
kura kwa kila mwananchi mpenda demokrasia na maendeleo katika jimbo
hilo.
Kanuni za kudhibiti misumeno ya moto zazinduliwa
WIZARA ya Kilimo na Maliasili imezindua kanuni ambazo zitadhibiti
matumizi ya misumeno ya moto kwa ajili ya kukabiliana na kasi ya
uharibifu wa mazingira inayotokana na ukataji wa miti uliokithiri.
Tanesco hakueleweki
PAMOJA na Shirika la Umeme (Tanesco) kudai kuwa kukatikakatika kwa umeme
kunakoendelea, kunatokana na shirika hilo kuzima mitambo ya Aggreko,
taarifa ya uzalishaji wa umeme kwenye Gridi ya Taifa, imeonesha kuwa
umeme unaozalishwa unatosha na kuzidi mahitaji.
Wabunge waagiza jenereta kwa mkurugenzi wa Tanesco lizimwe
KAMATI ya Hesabu za Mashirika ya Umma(POAC), imeagiza Bodi ya Shirika la
Umeme Tanzania (Tanesco) kuondoa jenereta la dharura lililopo nyumbani
kwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, William Mhando kuanzia leo ili naye
ajue machungu ya kukatika umeme mara kwa mara.
Mtei: Zitto haraka ya nini
MUASISI wa Chadema, Edwin Mtei ameamua kuvunja ukimya na kuzungumzia
kauli ya mbunge Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ya kutangaza nia ya
kugombea urais mwaka 2015.
Amekosoa uamuzi wa mbunge huyo kwa madai kwamba amefanya mapema mno kutangaza nia yake.
Amekosoa uamuzi wa mbunge huyo kwa madai kwamba amefanya mapema mno kutangaza nia yake.
CCM, Chadema jino kwa jino
KADRI uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki unavyokaribia, ndivyo vyama vyenye upinzani mkuu, CCM na Chadema vinavyozidi kukabana. Jana kwa vyakati tofauti, vyama hivyo viliendelea na kampeni zake maeneo mbalimbali ya jimbo hilo vikikusanya mamia ya wafuasi na wapenzi wake.
Wakati kampeni za Chadema zikiwa zinaongozwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, kwa upande wa CCM, Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde ndiye aliyeonekana kung'ara jana.
Upinzani waingia Ikulu Senegal
RAIS wa Senegal Abdoulaye Wade (85), ameangushwa vibaya na mpinzani wake, Macky Sall (50) katika duru ya pili ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika juzi.Matokeo hayo yamepokewa kwa hisia tofauti na wananchi wa Senegal na hata hapa nchini wengi wakisema anguko hilo la Wade ni somo kwa viongozi ving’ang’anizi wa madaraka barani Afrika.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wanasiasa, wasomi na wanaharakati nchini wamesema, anguko la Wade, linapaswa kuwa funzo kwa viongozi wanaokandamiza demokrasia katika nchi kadhaa barani Afrika.
Subscribe to:
Posts (Atom)