Monday, April 23, 2012
HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAKATI WA KUAHIRISHA MKUTANO WA SABA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA – DODOMA, TAREHE 23 APRILI 2012
UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika,
1. Nitumie nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema kwa kutuwezesha kutekeleza majukumu yote yaliyopangwa kwa ufanisi mkubwa katika Mkutano huu wa Saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioanza tarehe 10 Aprili 2012. Tumefanikiwa kufanya hivyo kutokana na maandalizi mazuri ya Mkutano, ushirikiano miongoni Mwetu na Waheshimiwa Wabunge wote kujiandaa vizuri katika kuchangia hoja mbalimbali zilizopangwa.
Mheshimiwa Spika,
2. Katika Mkutano huu, tumepata Waheshimiwa Wabunge Wapya Wawili wote kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Napenda kutumia nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Joshua Samwel Nassari kwa kuchaguliwa kuwa Mbunge Mpya wa Jimbo la Arumeru Mashariki. Vilevile, nampongeza Mheshimiwa Cecilia Daniel Paressokwa kuteuliwa kuwa Mbunge kupitia Viti Maalum (CHADEMA). Kipekee kabisa nawapongeza Wananchi wa Arumeru Mashariki kwa kutumia haki yao ya Kidemokrasia vizuri. Lakini kwa dhati kabisa, nakipongeza Chama Cha Mapinduzi kwa kukubali Matokeo ya Uchaguzi Mdogo wa Arumeru Mashariki. Kitendo hicho kinaonesha uungwana na ukomavu wa Kisiasa na Demokrasia katika Nchi yetu. Huu ni mfano mzuri wa kuigwa na Vyama vingine vyote vya Siasa Nchini.
3. Kwa Waheshimiwa Wabunge wapya tunawatakia mafanikio na tunawaahidi ushirikiano wetu ndani ya Bunge na katika Kujenga Taifa letu. Vilevile, napenda kutumia nafasi hii pia kuwapongeza Waheshimiwa Madiwani wote waliopata Ushindi katika Chaguzi zilizofanyika katika Kata za Vijibweni (Temeke), Kiwangwa (Bagamoyo), Kirumba (Mwanza), Logangabilili (Bariadi), Chang’ombe (Dodoma), Kiwira (Rungwe), Lizaboni (Songea) na Msambweni (Tanga). Tunawatakia wote waliochaguliwa afya njema na maisha mazuri ili muweze kuwatumikia Wananchi waliowachagua na Taifa kwa ujumla.
Zitto aomba Bunge la dharura kumjadili Pinda
Leo wakati Zitto anawasilisha hoja yake ya kutaka kura ya kutokuwa na
imani na Waziri Mkuu pamoja na kuiwasilisha misingi ya maombi yake
ametumia kanuni ya 27(4) ambayo inataka kuitishwa kwa Bunge la dharura
na mwenye mamlaka hiyo ni Spika wa Bunge .
Kanuni hiyo inasema kama ifuatavyo; "Endapo manufaa ya Taifa yatahitaji kuwa Bunge lisikutane tarehe ile iliyowekwa kwa Mkutano utakaofuata,bali likutane tarehe ya mbele zaidi au ya nyuma zaidi,basi Spika anaweza ,baada ya kushauriana na Kamati ya Uongozi ,kuliita Bunge likutane tarehe hiyo ya mbele au nyuma zaidi"
Kifungu hicho kimetumiwa na hivyo kwa kuwa Waziri Mkuu katangaza Bunge kukutana tarehe 12/06/2012 basi kuna uwezekano mkubwa likakutana mapema zaidi ili kujadili hoja hiyo.
Msingi mwingine wa hilo ni kutokana na ukweli kuwa kitendo cha waziri mkuu kuendelea kuwa ofisini huku akijua kuwa bunge linaweza kumjadili wakati wowote kinamfanya akose ujasiri wa kufanya maamuzi ama kuweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na hivyo kudidimiza uchumi wa taifa , au hata kufanya maamuzi akijua kuwa wakati wowote anaweza kuondolewa.
naomba kuwasilisha.

Nicolas Sarkozy apoteza awamu ya kwanza ya uchaguzi
French President Nicolas
Sarkozy faces an uphill struggle in the second round of the presidential
election, after coming second in Sunday's first vote.
He won 27.1% of the vote, while his Socialist rival Francois
Hollande took 28.6%, the first time a sitting president has lost in the
first round.KESI YA LULU YATAJWA KWA MARA YA PILI LEO MAHAKAMA YA KISUTU
Mshatkiwa
Elizabeth Michael |(17), ' Lulu' akielekea kupanda ngazi na
kupandishwa Kizimbani Kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa Upelelezi
haujakamilika hiyo ni kwa mujibu wa Wakili wa Serikali Elizabeth
Kaganda alisema mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Rita Tarimo
hivyo kesi hiyo itatajwa tena Mei 7 mwaka huu. Mtuhumiwa amerudishwa rumande.
Akisindikizwa .
Mshtakiwa akipanda ngazi kuelekea
Kizimbani ambalo kesi yake ilitajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu Jijini Dar es Salaam huku akiwa katika ulinzi kutoka kwa askari
Magereza.
Tofauti na ilivyokuwa alivyo pandishwa
kizimbani kwa mara ya kwanza 'Lulu' leo alikuwa katika ulizni wa hali
ya juu huku askari magereza wakiwa wamevalia mikanda yenye mabomu ya
machozi ikiwa ni katika kukabilia na rapsha ya aina yeyote ambayo
ingeweza kutokea .
Kitu kingine ni kwamba msanii huyo alifika akiwa
amevalia gauni refu na mtandio wake mwekundu walitu walijaa lakini siyo
kwa wingi ambao wengi walitarajia kutokana na umaarufu alio nao Lulu
hata kabla ya kufikwa na tuhuma hizo za kesi ya mauaji ya aliyekuwa
Msanii nyota wa Filamu nchini Steven Charles Kanumba.
FATAKI AFUMANIWA AKIW ANA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI
Alikuwa na gari ya serikali
WAKATI serikali na taasisi mbalimbali zikihamasisha kuwalinda wanafunzi kutoka kwenye mikono ya wanaume wanaofanya mapenzi na wanafanzi, ‘mafataki’, Mustafa Kachenga (39), mkazi wa Kiluvya, jijini Dar es Salaam amenaswa gesti (jina tunalo) akiwa na mwanafunzi wa kidato cha pili.NI ASUBUHI SIKU YA KAZI
Tukio hilo la aibu ambalo lilishuhudiwa na baadhi ya majirani, lilijiri saa tano asubuhi ya Aprili 16, 2012 ndani ya gesti hiyo maarufu iliyopo Manzese, jijini Dar es Salaam.
Habari zinasema, Kachenga ni dereva wa kigogo mmoja Wizara ya Ujenzi na kwamba, siku ya tukio alimpeleka bosi wake huyo kwenye semina na kumwacha kwa maelekezo ya kumrejea jioni.
POLISI, MAPAPARAZI WAINGIA KAZINI
Mara baada ya kupata taarifa hizo, timu yetu ya mapaparazi ilifunga safari mpaka Kituo cha Polisi Urafiki, Ubungo na kutoa taarifa ambapo askari watatu wasiokuwa na sare walitolewa kwa ajili ya msafara wa kwenda kumnasa fataki huyo.
Kwa kutumia msaada mkubwa wa chombo hicho cha dola, uongozi wa gesti hiyo ulipewa taarifa, chumba namba tano kikagongwa na kufunguliwa na mwanaume huyo aliyejitupia taulo kama yuko kwake Kiluvya ambapo aliwekwa chini ya ulinzi.
Mwanafunzi huyo anayesoma Sekondari ya Kiluvya, alikutwa akiwa mtupu juu ya kitanda, alishtuka kwa ugeni wa ghafla na kuanguka sakafuni akijifanya amepoteza fahamu ingawa haikuwa kweli.
ETI MWANAUME AJITETEA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwanaume huyo aliyekuwa na gari la serikali namba STK alipobanwa kuhusu uwepo wake na mwanafunzi ndani ya gesti hiyo alisema amekuwa akimsaidia kumsomesha hivyo na yeye huwa ‘anasaidiwa mambo f’lani’.
Hata hivyo, jamaa huyo akaapa kuwa hatarudia tena baada ya kuligundua kosa huku, kama kawaida ya binadamu, akimlaumu shetani kuwa ndiye aliyemdanganya.
DENTI KILIO MUDA WOTE
Wakati mpenzi wake huyo akitaitiwa na maswali ya awali, mwanafunzi huyo mwenye miaka 16 alikuwa akichuruzika machozi muda wote.
SAFARI YA KITUONI
Maafande shupavu waliwatwaa wawili hao ndani ya usafiri wao sanjari na mapaparazi wetu mpaka Kituo cha Polisi cha Magomeni ambako walitoa maelezo na baadaye kuswekwa mahabusu kwa kila mmoja na jinsi yake.
PAMOJA NA TETESI ZINAZOENDELEA SAJUKI BADO MZIMA INGAWA HALI YAKE YA KIAFYA SIO NZURI
UKWELI ni kwamba, staa mkubwa wa filamu za Kibongo, Sadick Juma
Kilowoko ‘Sajuki’ anaumwa,
Hali ya Sajuki imeendelea kuwa mbaya akidhoofu mwili siku hadi siku kutokana na kusumbuliwa na tatizo la uvimbe tumboni kwa muda mrefu sasa.
Aprili 15, mwaka huu Sajuki na mkewe Wastara Juma walifanya sherehe ya 40 ya kumtoa mtoto wao, Farheen ambayo ilihudhuriwa na waandishi wetu waliomshuhudia msanii huyo akiwa amedhoofu sana.

Pichani juu: Sadick
Juma Kilowoko ‘Sajuki’ (mwenye miwani) akiwa katika sherehe ya 40 ya
kumtoa mtoto wao, Farheen iliyofanyika Aprili 15, mwaka huu.
Kwa mujibu wa mkewe Wastara, Sajuki alipokwenda katika Hospitali ya Apollo nchini India hivi karibuni alipewa dawa za kutumia kwa muda ambapo mwezi ujao (Mei) alitakiwa kurejea tena nchini humo kwa ajili ya matibabu zaidi.
Hali ya Sajuki imeendelea kuwa mbaya akidhoofu mwili siku hadi siku kutokana na kusumbuliwa na tatizo la uvimbe tumboni kwa muda mrefu sasa.
Aprili 15, mwaka huu Sajuki na mkewe Wastara Juma walifanya sherehe ya 40 ya kumtoa mtoto wao, Farheen ambayo ilihudhuriwa na waandishi wetu waliomshuhudia msanii huyo akiwa amedhoofu sana.
Kwa mujibu wa mkewe Wastara, Sajuki alipokwenda katika Hospitali ya Apollo nchini India hivi karibuni alipewa dawa za kutumia kwa muda ambapo mwezi ujao (Mei) alitakiwa kurejea tena nchini humo kwa ajili ya matibabu zaidi.
Sunday, April 22, 2012
JACOB ZUMA AOA MKE WA SITA, NI BONGI NGEMA
RAIS wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, jana Jumamosi ameoa mke wa sita
katika sherehe ya siku ya pili iliyopambwa kwa shamra za kabila la
Wazulu. Rais huyo mwenye umri wa miaka 70 alimwoa Bongi Ngema siku ya
Ijumaa katika mvumo wa nyimbo za Kizulu akiwa amevaa ngozi ya chui na
kubeba ngao huku akiwa amezungukwa na wanaume waliokuwa wamvalia nguo za
wapiganaji wa kijadi.
Msimamizi wa ndoa hiyo alikuwa ni mke wa nne wa Zuma aitwaye Nkandla katika sherehe iliyofanyika KwaZulu-Natal na kufuatiwa na sherehe za kisasa ambazo zilikuwa ni pamoja na kukata keki.
Msimamizi wa ndoa hiyo alikuwa ni mke wa nne wa Zuma aitwaye Nkandla katika sherehe iliyofanyika KwaZulu-Natal na kufuatiwa na sherehe za kisasa ambazo zilikuwa ni pamoja na kukata keki.

Rais Jacob Zuma na mkewe Bongi Ngema wakikata keki.

...Wakiwa na nyuso za tabasamu.
...Hapa ni wakati wa ndoa ya kimila.
Zuma akiwa amevaa ngozi ya chui na kubeba ngao wakati wa harusi ya kimila.
...Harusi ya kimila ikiendelea.
Zuma na Ngema wana mtoto wa miaka saba wa kiume. Ndoa hiyo ni ya tatu katika miaka minne iliyopita naya pili tangu ashike urais wa nchi hiyo mwaka 2009 akiwa rais mwenye wake wengi.
Kiongozi huyo ameoa mara sita na ana watoto 21 ambapo mmoja wa wake zake amekufa na mwingine ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Nkosazana Dlamini-Zuma – ametalikiana naye. Wanawake hao hufaidika kwa kusafiri na rais huyo na kufanya kazi za ukatibu mahsusi, pamoja na kufuatana naye katika ziara za kiserikali.
Pamoja na kwamba Zuma aligharimia ndoa hiyo yeye mwenyewe, serikali pia imeongeza bajeti yake maradufu kwa zaidi ya Dola milioni mbili kutokana na kumwoa mwanamke huyo akiwa mmoja wa familia yake.
Hata hivyo, ndoa ya wanawake wengi inaonekana kupoteza umaarufu nchini Afrika Kusini ambapo ustaarabu wa nchi za Magharibi unazidi kuota mizizi ambapo idadi kubwa ya watu wa nchi hiyo hawakubaliani na utamaduni huo hivi sasa.
RAIS KIKWETE AOMBOLEZA KIFO CHA BRIGEDIA JENERALI MWAKANJUKI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein kufuatia kifo cha mwanasiasa mkongwe Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki aliyefariki dunia katika Hospitali Kuu ya Jeshi, Lugalo jijini Dar-es-Salaam jana tarehe 19 April, 2012.
Marehemu amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi visiwani Zanzibar zikiwemo za Uwaziri katika Wizara mbalimbali na pia kuwahi kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.
"Pokea rambirambi zangu za dhati kwa kuondokewa na mzee wetu, kiongozi shupavu na mwanamapinduzi imara, ni pengo kubwa kwetu kwani Marehemu amekuwa mshauri wetu mkweli na muwazi, upendo na ucheshi wake pia ilikuwa faraja kwetu wakati wa vipindi vigumu na vyepesi" Rais ameeleza,
"Tutaukosa ushauri wake, upendo wake na mchango wake katika kila hali" Rais amesema na kumuomba Rais Dk. Ali Mohamed Shein kufikisha salamu zake za rambirambi kwa familia, wananchi wote na viongozi wenzake ambao marehemu amefanya nao kazi katika idara zote serikalini, jeshini, na pia katika Baraza la Wawakilishi.
Rais Jakaya Kikwete akitoa heshima za
mwisho kwa Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki mapema
asubuhi leo Aprili 22, 2012 katika kambi ya JWTZ ya Kikosi cha Anga
kabla ya kupelekwa Zanzibar kwa mazishi.…
Rais Jakaya Kikwete akitoa heshima za
mwisho kwa Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki mapema
asubuhi leo Aprili 22, 2012 katika kambi ya JWTZ ya Kikosi cha Anga
kabla ya kupelekwa Zanzibar kwa mazishi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mkuu wa
Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange na Mhe. Aboud wakiangalia wakati
jeneza lenye mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki
ulipokuwa unaingizwa katika ndege mapema asubuhi leo Aprili 22, 2012
katika kambi ya JWTZ ya Kikosi cha Anga kabla ya kupelekwa Zanzibar kwa
mazishi.
PICHA NA IKULU
Marehemu Mwakanjuki alianza siasa kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 akianzia katika Chama Cha Afro Shiraz (ASP) na baadae Chama cha Mapinduzi.
"hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwa mchango wa marehemu wakati wa uhai wake nasi twamuombea mapumziko mema ya milele, Amina" Rais amemuombea Dua na kuiomba familia ya marehemu kuwa na subira wakati huu wakuondokewa na mpendwa wao.
MANCHESTER UNITED 4, EVERTON 4
Mshambuliaji wa Manchester United,
Wayne Rooney (kulia) akishangilia na wenzake baada ya kufunga bao la nne
dhidi ya Everton katika mechi yao iliyopigwa kwenye Uwanja wa Old
Trafford jijini Manchester, England leo. Timu hizo zimetoka sare ya 4-4.
Kiungo wa Everton Steven Pienaar
(kushoto) akiifungia timu yake bao la nne dhidi ya Manchester United leo
kwenye Uwanja wa Old Trafford jijini Manchester, England.
(PICHA NA AFP/Getty…

HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU BUNGENI KWA MUJIBU WA KATIBA IBARA YA 53A NA KANUNI YA BUNGE, KIFUNGU CHA 133 KUWASILISHWA KWA SPIKA LEO
Masharti yametimizwa; wabunge 73 wazalendo wamesaini
Ni mwendelezo wa ‘operesheni uwajibikaji’Mnamo tarehe 19/04/2012 wakati nahitimisha hoja ya Kamati ya Mashirika ya Umma nilieleza kusudio langu la kuwaomba waheshimiwa wabunge waniunge mkono katika kutia saini zisizopungua asilimia 20 ya wabunge wote ili kuweza kutimiza matakwa ya Katiba ibara ya 53A kwa ajili ya kuwasilisha Bungeni hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.
Mnamo tarehe 20/04/2012 niliandaa orodha ya waheshimiwa wabunge wote na kuisambaza ndani na nje ya ukumbi wa Bunge ili waheshimiwa wabunge wote waweze kutia saini hizo, na mpaka leo tarehe 22/04/2012 orodha hiyo imetimiza idadi ya wabunge wazalendo wanaopigania uwajibikaji 73 kutoka vyama vyote vyenye uwakilishi Bungeni, isipokuwa chama cha UDP ambacho kina Mbunge 1 na hajatia saini waraka huo mpaka sasa.
Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kifungu cha 133 (1) kinasomeka “Mbunge yeyote anaweza kutoa taarifa ya maandishi kwa Spika ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 53A ya Katiba” na kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (3) kinasomeka “hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haitajadiliwa na Bunge isipokuwa tu kama;
“taarifa ya maandishi iliyowekwa saini na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote itatolewa kwa Spika, siku zisizopungua kumi na nne kabla ya siku inayokusudiwa kuwasilishwa Bungeni;”
Hali kadhalika kanuni za Bunge Kifungu cha 133 (4) kinasomeka kuwa “hoja inayotolewa chini ya Kanuni hii na iliyotimiza masharti ya Katiba,itawasilishwa Bungeni mapema iwezekanavyo na itaamuliwa kwa kura za siri”.
Hivyo basi baada ya kutimiza matakwa ya kikatiba na kanuni za Bunge leo tarehe 23/04/2012 nitawasilisha rasmi kwa Spika Taarifa ya Maandishi kwa mujibu wa kanuni 133 (1) na (3) ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa kushindwa kusimamia uwajibikaji wa Serikali bungeni kwa mujibu wa ibara ya 52 na hivyo kulinda mawaziri wenye kusababisha matumizi mabaya ya fedha za umma na kulisababishia hasara taifa.
Tunatarajia kwamba siku kumi na nne baada ya kuwasilisha hoja hiyo bunge litakutana kwa haraka kujadili hoja hiyo ili kuwezesha uwajibikaji na hatua kuchukuliwa za kuhakikisha mapendekezo ya ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na maazimio ya Bunge yanatekelezwa. Hoja hii ni mwendelezo wa ‘operesheni uwajibikaji’ hivyo tunaomba wabunge na watanzania wote waiunge mkono ili kunusuru uchumi wa nchi na kuchangia katika ustawi wa wananchi.
Kwa niaba ya wabunge waliotia saini kuunga mkono taarifa ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu;
…………………………….
Kabwe Zuber Zitto.Mbunge Jimbo la Kigoma Kaskazini.
22/04/2012.
Kamati yapendekeza wabunge watungiwe kanuni za maadili
KAMATI ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imependekeza wabunge
watungiwe kanuni zinazohusu maadili ya wanasiasa hao ambazo zinaweka
viwango kwa mienendo ya wabunge pale watakapokuwa wakitekeleza majukumu
yao ya kibunge wawapo nje na katika eneo la Bunge.
Kamati hiyo inaeleza kuwa kwa sasa maadili ya wabunge ambayo yanasimamiwa kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, ambayo kwa madhumuni ya usimamizi bora wa maadili ya wabunge, sheria hiyo haikidhi haja ikiachiwa itumike peke yake.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hassan Ngwilizi, kwenye taarifa hiyo anaeleza kuwa uzoefu unaonesha kuwa baadhi ya mabunge katika Jumuiya ya Madola tayari wana kanuni za maadili na mwenendo wa wabunge ambazo utafiti unaonesha kuwa kwa kiasi fulani kuwepo kwa kanuni hizo
kunaongeza imani ya wananchi kwa mabunge yao.
Malengo mengine ni kuwafanya wabunge kuonesha viwango vya juu vya maadili katika kutekeleza majukumu ya umma hususani wanapokuwa wakiisimamia Serikali.

Bunge lakamilisha kusikiliza mashauri ya Masaburi, Mdee
MALALAMIKO ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Philip Mangula dhidi ya
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) na shauri linalomhusu Meya wa Jiji
la Dar es Salaam, Didas Masaburi anayetuhumiwa kuwatukana wabunge kuwa
wanafikiri kwa kutumia makalio, yamemalizika kusikilizwa na Kamati ya
Bunge.
Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge katika taarifa yake ya utekelezaji kwa mwaka 2011/12 iliyowekwa mezani mwishoni mwa wiki katika Mkutano wa Saba wa Bunge unaoendelea mjini hapa, inaeleza kuwa kamati imemaliza kusikiliza mashauri hayo na uamuzi wameupeleka kwa Spika Anne Makinda.

Tanesco taabani
BUNGE limeelezwa kuwa hali mbaya inayolikabili Shirika la Umeme (Tanesco)
imefanya shirika hilo kusimamisha huduma yake ya kuwaunganishia wateja
wapya umeme.
Lengo la Serikali ni kufikia walau asilimia 30 ya kaya za Watanzania wanaotumia umeme
ifikapo mwaka 2015 na ili kufikia lengo hilo, ilikadiriwa kuwa ni lazima Tanesco iunganishe wateja wapatao 137,000 kwa mwezi kuanzia Machi 2012.
“Kutokana na hali mbaya ya kifedha na kiuendeshaji wa shirika, lengo hili halitaweza kufikiwa
kwani Tanesco inashindwa kulipia vifaa vya kutosha kwa wakati,” alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, January Makamba.

Nundu asigana na Naibu wake
WAZIRI wa Uchukuzi, Omar Nundu amesema anapigwa vita na Naibu Waziri wake, Athumani
Mfutakamba baada ya yeye kupinga Kampuni ya CCCC kupewa zabuni ya kupanua Bandari ya Dar es Salaam.
Akizungumza jana na waandishi wa habari mjini hapa, Nundu alisema CCCC iliwahi kwenda kumshawishi yeye ili akazungukie katika nchi mbalimbali kutembelea miradi ya kampuni hiyo, lakini alikataa kwa vile alijua kuwa kufanya hivyo ni kama hongo.
Nundu alisema lakini cha ajabu, Naibu Waziri wake alipofuatwa na kampuni hiyo, alikubali na akapelekwa kwenye nchi za Mauritius, China na Guinea Bissau bila hata kumtaarifu bosi wake.

Mbivu za Jairo, mawaziri leo
SERIKALI leo inaweka wazi bungeni ni namna gani imemwajibisha aliyekuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo ambaye alitiwa
hatiani na Kamati Teule iliyomchunguza juu ya uchangishaji fedha kwa
ajili ya kupitisha bajeti bungeni.
Aidha, Mkutano wa Saba wa Bunge la 10 unaahirishwa leo huku macho na masikio yakiwa kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wakitaka kufahamu hatima ya mawaziri wanaoshinikizwa kujiuzulu kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni ama kuhusika au kushindwa kudhibiti ubadhirifu wa fedha za umma.
Kuhusu sakata la Jairo, taarifa ya Serikali juu ya utekelezaji wa maazimio ya Kamati Teule iliyotaka Jairo awajibishwe, itawasilishwa mezani kwa maana haitasomwa na wala kujadiliwa
na wabunge.

Subscribe to:
Posts (Atom)