Leo wakati Zitto anawasilisha hoja yake ya kutaka kura ya kutokuwa na
imani na Waziri Mkuu pamoja na kuiwasilisha misingi ya maombi yake
ametumia kanuni ya 27(4) ambayo inataka kuitishwa kwa Bunge la dharura
na mwenye mamlaka hiyo ni Spika wa Bunge .
Kanuni hiyo inasema kama ifuatavyo; "Endapo manufaa ya
Taifa yatahitaji kuwa Bunge lisikutane tarehe ile iliyowekwa kwa Mkutano
utakaofuata,bali likutane tarehe ya mbele zaidi au ya nyuma zaidi,basi
Spika anaweza ,baada ya kushauriana na Kamati ya Uongozi ,kuliita Bunge
likutane tarehe hiyo ya mbele au nyuma zaidi"
Kifungu hicho kimetumiwa na hivyo kwa kuwa Waziri Mkuu katangaza Bunge
kukutana tarehe 12/06/2012 basi kuna uwezekano mkubwa likakutana mapema
zaidi ili kujadili hoja hiyo.
Msingi mwingine wa hilo ni kutokana na ukweli kuwa kitendo cha waziri
mkuu kuendelea kuwa ofisini huku akijua kuwa bunge linaweza kumjadili
wakati wowote kinamfanya akose ujasiri wa kufanya maamuzi ama kuweza
kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na hivyo kudidimiza uchumi wa taifa
, au hata kufanya maamuzi akijua kuwa wakati wowote anaweza kuondolewa.
naomba kuwasilisha.
No comments:
Post a Comment