Hatumwi
mtoto dukani. Ni msemo uliowahi kuusikia mara nyingi, lakini siku ya jumatatu
utakua sahihi.
Ni siku
ambapo wababe wawili wa Ligi kuu ya Premier ya England watapambana ikiwa ni
kwenye uwanja wa Etihad wa Manchester City.
Baina ya
timu hizi zimefunga bao 173 katika Ligi msimu huu tukishuhudia mengi
yaliyofungwa na Wayne Rooney, Sergio Aguero, Javier Hernandez na Carlos Tevez.
Majina
haya yanakupa ufahamu kua kila upande unaweza kufanikiwa kuchota pointi kutoka
uwanja wa Etihad na kwa ushindi apo Etihad pia Ligi ya msimu huu.
Ukitazama
orodha ya majina utaingiwa na tamaa ya ya pambano la kuvutia kutokana na
washambuliaji wenye mikwaju mikali bila kusahau wanaowalisha mipira ya kupasua
nyavu.
Man.City
kwa kipindi kirefu imemtegemea David Silva na bado anaweza kushawishi matokeo
ya mechi wakati wowote huku United ikimtegemea mno Antonio Valencia aliyekua na
ushawishi mkubwa msimu huu kwa kuvunja ngome nyingi za vilabu mbalimbali.
.
Vijana wa
Roberto Mancini walipoteza muelekeo baada ya siku kuu ya Krisimasi kipindi
ambapo kiwango cha mcheza kiungo David Silva kilianza kushuka ingawa hivi sasa
klabu yake imerejesha uwezo wa kufunga mabao kutokana na hali yake kua bora kwa
sasa.
Na huku
kurejea kwa mshtuko kwa Paul Scholes mwezi januari kunaweza kuonekana kama
changamoto iliyoiwezesha United kupanda kilele cha Ligi kuu, ingawa mchango wa
Valencia kutoka upande wa kulia ni mkubwa mno. Valencia.
Kufuatia
jeraha la kisiginio la mda mrefu mapema msimu huu Valenzia alizinduka kwa
kupachika wavuni bao mbili kati ya 4-1 dhidi ya Wolves tarehe 10 Disemba.
Kwa
uchache, hawa ni wawili kati ya orodha ndefu ya wachezaji wa Manchester mbili
zinazotambiana kushinda pambano la jumatatu litakaloamua mshindi wa Ligi ya
mwaka huu.
Tuangalie
uwezekano wa hali inayoweza kujitokeza ikiwa kwa mfano:
City
itashinda - basi timu hizi mbili zitakua sawa kwa pointi kukisalia mechi mbili,
wingi wa goli za City ukiiweka klabu hio juu ya kilele.
Droo -na
hapa United itahitaji pointi nne kutoka mechi zilizobaki, hata ikiwa City
itashinda mechi zote zilizobaki.
Hapa
ushindi wa United katika mechi itakayofuata dhidi ya Swansea basi itatangazwa
United kua mshindi endapo City itashindwa kuifunga Newcastle ugenini.
Endapo
United itashinda pambano la jumatatu basi Ligi itahesabu kombe la 20 la United.
No comments:
Post a Comment