Monday, April 30, 2012

Auawa kwa risasi akivamia shamba

WILAYA ya Arumeru imeendelea kukumbwa na matukio ya vifo baada ya mwananchi mmoja mwenye miaka kati ya 25 na 30, ambaye jina lake halijafahamika, kuuawa kwa kupigwa risasi na walinzi wa shamba la Mitomiwili lililoko Kilala, kata ya Sing’isi, Tengeru.

Mauaji hayo yametokea ikiwa ni siku moja baada ya kuuawa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kata ya Usa River, Msafiri Mbwambo.

Mpaka sasa idadi ya watu waliokufa kwa kipindi cha wiki moja katika matukio ya kutatanisha ni sita baada ya vijana wengine wanne kukutwa wamekufa na miili yao kutupwa kwenye maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye, alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa nne usiku wakati marehemu akiwa na kundi la wananchi wengine wanaokadiriwa kuwa kati ya 40 na 50 ambao walivamia shamba hilo la mwekezaji.

Alisema kuwa mwananchi mwingine ambaye pia jina lake halikupatikana mara moja alijeruhiwa vibaya na anapatiwa matibabu chini ya ulinzi wa polisi.

Kamanda huyo alifafanua kuwa walinzi hao wa shamba hilo ambao hakuwataja kwa majina walimuua marehemu huyo kwa kutumia bunduki aina ya shortgun wakati wa kulinda mali za tajiri yao.

Andengenye aliongeza kuwa wananchi hao baada ya kuvamia shamba hilo linalomilikiwa na kampuni ya Pulse and Agrocommodities, waliharibu mali kwa kuchoma matrekta manne, kuiba mifuko ya mbolea 300 huku wakivunja vioo vya gari lililokuwa limeegeshwa eneo hilo ambapo thamani halisi ya mali zilizoharibiwa bado haijajulikana.

Hata hivyo alisema kuwa mpaka sasa hakuna mtu anayeshikiliwa na polisi kuhusiana na matukio hayo licha ya jeshi hilo kuendelea na uchunguzi.

Sunday, April 29, 2012

Pamoja na Kuugua Sajuki aendelea kupiga mzigo

Licha ya kwamba afya ya msanii wa filamu za Kibongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ bado hairidhishi kutokana na maradhi yanayomsumbua, juzikati staa huyo na mkewe Wastara Juma walinaswa ‘lokesheni’ wakiendelea kurekodi filamu yao.

 

Sajuki amekiri kuwa afya yake bado siyo nzuri lakini ameona badala ya kukaa ndani ni vyema akajishughulisha ili kukabiliana na ugumu wa maisha.
“Bado hali yangu si nzuri lakini kama mtu unaumwa na huna kitu kingine cha kukusaidia katika maisha lazima uwajibike, naumwa lakini siwezi kukaa nyumbani kwa sababu kila dakika moja ya maisha yangu inahitaji fedha,” alisema Sajuki.
 

Naye Wastara alisema kuwa, afya ya mumewe bado hairidhishi ndiyo maana wameamua kuingia mzigoni ili kuhakikisha wanapata fedha kwa ajili ya matibabu.
 “Kama unavyomuona mume wangu, kimsingi anaumwa na zinahitaji fedha kwa ajili ya matibabu yake na kujikimu pia, ndiyo maana unatuona tumeamua kuendelea na shughuli zetu za kisanii kwani bila kufanya hivi tutakwama katika mambo mengi.
 
“Hata hivyo, bado tunahitaji msaada ili tuweze kufanikisha matibabu ya Sajuki ambaye tunatarajia kumpeleka India haraka iwezekanavyo,” alisema Wastara.

Mkurugenzi BoT kusubiri maelezo ya kesi

Kesi yaahirishwa hadi Mei 30 mwaka huu


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kumsomea maelezo ya awali Naibu Mkurugenzi wa Mifumo na Huduma wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Simon Jengo, anayetuhumiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi kwa kununua mashine 26 za kuharibu noti kutokana na mawakili wa Takukuru kutokuwepo mahakamani.

Kesi hiyo ilikuja jana kwa ajili ya kuanza kusoma maelezo ya awalilakini Hakimu Mkazi, Ritha Tarimo aliiahirisha kwa sababu mawakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) walikuwa na udhuru.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Tarimo aliiahirisha hadi Mei 30 mwaka huu kwa ajili ya mshtakiwa huyo kusomewa maelezo ya awali yanayohusiana na shtaka hilo linalomkabili.
Awali, akisoma hati ya mashitaka, Mwendesha Mashitaka wa Takukuru,  Ben Lincon alidai mshtakiwa alitenda makosa hayo kati ya Januari 2005 na Desemba 2008 makao makuu ya BoT.

Alidai kuwa mshtakiwa alimshauri vibaya Gavana wa BoT katika ununuzi wa mashine 26 za kuharibu noti pasipo kujali mahitaji halisi ya benki.

Mshitakiwa yuko nje kwa dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika watakaosaini dhamana ya maneno ya Sh10 milioni kila mmoja.

Jengo pia anakabiliwa na kesi nyingine katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala ambapo anashtakiwa na maofisa wengine watatu wa BoT akidaiwa kughushi nyaraka kwa kampuni inayotengeneza noti za benki hiyo kwa lengo la kumdanganya mwajiri wao.

Washtakiwa wengine ni Kisima Mkango, Bosco Kimela na Ally Farjallah Bakari ambao kwa pamoja wanadaiwa kutenda makosa hayo jijini Dar es Salaam. 



Wanadaiwa kuwasilisha nyaraka kwa kampuni hiyo ili kuchapisha kiasi kikubwa cha noti tofauti na kilichoidhinishwa na mwajiri wao.

Katika mashtaka mengine wanadaiwa kuingia mkataba wa kuchapa noti kwa bei ya juu kinyume na makubaliano halali hivyo kuisababishia Serikali hasara ya Sh104,158,536,146. 


Wanadaiwa pia kuupeleka mkataba huo kwa mamlaka zinazotengeneza noti ukionyesha gharama za uongo

Friday, April 27, 2012

Ethiopia kula nyama mbichi ni jambo la kawaida.

Maeneo mengi katika nchi ya Ethiopia ni jambo la kawaida. .










Maandalizi huanzia buchani. Nyama ya Mbuzi na Ngamia hukatwa katwa vizuri na kuchanganywa na Viuongo tu, kisha huwa tayari kwa kuliwa kama inavyoonekana katika picha hapo juu.

Furaha yamtoa Tundu Lissu Machozi



Wakili wa waleta maombi ya wana CCM, Godfrey Wasonga, akitafakari kwa hisia kali muda mfupi kabla ya kesi ya kupinga matokeo yaliyompa Ubunge Tundu Lissu, hayajatangazwa leo Mahakamani. (Picha zote na Nathaniel Limu)



Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki CHADEMA,Tundu Lissu, akilia kwa furaha muda mfupi baada ya Mahakama Kuu, kutupilia mbali maombi yaliyotolewa na Shaban Selema na Pascal Halu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupinga watokeo yaliyompa ushindi wa Ubunge, Mbunge huyo.



 Mbunge wa viti maalum Kataru, mkoani Manyara, Rose Kamili (anayeangaalia kamera), akilia kwa furaha pamoja na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu, muda mfupi baada ya Mahakama Kuu, kutupilia mbali pingamizi la kupinga matokeo yaliyompa ushindi wa Ubunge, Tundu Lisu,  leo mkoani humo


Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu, akifutwa machozi na mke wake, wakati wakitoka nje ya Mahakama Kuu, baada ya Mahakama hiyo, kutangaza kuwa ushindi wake huo ni halali.


Baadhi wa watu waliohudhuria kusikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Tundu Lisu kuwa Mbunge, wakifurahia ushindi huo, muda mfupi baada ya maamuzi hayo kutolewa.
.