Tuesday, March 27, 2012

Mashahidi kesi ya Tundu Lissu watoweka

Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge wa jimbo la Singida Mashariki, iliyofunguliwa katika Mahakama Kuu, jana iliingia kasoro baada ya upande wa walalamikaji kukosa mashahidi.

Kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Moses Muzuna, asubuhi ilihojiwa shahidi Sophia Abdala Mhoji ambaye ni shahidi wa tano, Mateo Cosmas Mnyambii ambaye ni shahidi wa sita kabla ya jaji hajaahirisha kesi hadi majira ya mchana.

Hata hivyo, katika hali isiyo ya kawaida, kesi iliporejea tena mchana wakili wa walalamikaji, alisimama kumwomba jaji aahirishe kesi mpaka leo kufuatia shahidi aliyepaswa kuingia kutoonekana, na mwingie aliyekuwepo akidaiwa hajajipanga vema.

Wakili Wasonga: Mashahidi wengine wanaotoka kijijini wamerudi, na huyu anayekaribu inaelekea ataongea vitu visivyo vya msingi. Naomba kesi iahirishwe hadi kesho tukajaribu kujipanga.

Lissu alisimama na kusema: “Sitaki kumfundisha wakili namna ya kuendesha kesi yake. Wakili alipaswa kujua kuwa hajui kuwa mashahidi wake anaowaleta wanakuja kuzungumza mambo yasiyo ya msingi.

Nashindwa kuelewa kwa nini walimfanya mtu kuwa shahidi wakati wanajua hajui kinachobishaniwa mahakamani. Kutokana na ucheleweshaji huu, wakili wa walalamikaji, wabebe gharama za kesi. Kwa nini waliomba turudi mchana kama walikuwa hawajajiandaa?

Jaji: Ni vizuri wakili wa walalamikaji atumie muda mzuri, uwe unawaandaa mashahidi wako. Ila kwa sasa kwa kuwa tumeshasikiliza mashahidi wa asubuhi, naomba walalamikiwa wasibebe gharama ila ikijirudia mahakama itajua namna ya kuchukua hatua stahiki.

No comments:

Post a Comment